Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka mjini Zanzibar, zinaeleza kuwa yule Mtu anayesadikika kudaiwa kumuua Padr Evalist Mushi wa Kanisa Katoliki lililopo Visiwani Zanzibar siku za hivi karibuni, amekamatwa leo akiwa katika maeneo ya Kariakoo mjini Zanzibar.
Imeelezwa na Ripota wa Mtandao huu kuwa Jeshi la Polisi la Mjini Unguja, tayari limethibitisha tukio hilo la kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment