Mchezaji wa Timu ya Ikulu ya Zanzibar, Ali Mwinyi (kulia) akichuana kuwania mpira na Shaaban Kasanga wa Timu ya ikulu Dares Salaam, wakati wa mchezo wa Kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya Pasaka. Katika mchezo huo Ikulu Zanzibar iliibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Mchazaji wa Timu ya mpira wa mikono Netball ya Ikulu ya Dar es Salaam, Haika Masoud, akimzuia Beshuu Abdallah, wa Ikulu ya Zanzibar,wakati wa Mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye viwanja vya Amani Nje mjini Zanzibar leo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya Pasaka. Katika mchezo huo Ikulu Zanzibar iliifunga Ikulu ya Dar es Salaam kwa vikapu 26-14.Picha na Ramadhan
Othman Ikulu


No comments:
Post a Comment