Mshauri wa
Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Liu Dong, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu manufaa ya ujio wa Rais wa China, hali
ya mkutano wa kwanza wa Bunge la umma ya 12 la China pamoja na mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauriano
ya kisiasa la awamu ya 12 la China. Pia China imeishukuru serikali ya Tanzania
kwa mapokezi mazuri wakati wa ziara ya Rais mpya XI Jinping ya
Jamhuri ya Watu wa China, pamoja na
waandishi wa habari katika juhudi zakuendeleza uhusiano mzuri baina ya
China na Tanzania.
Mkalimali kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jack Yu akitoa taarifa kwa wanahabari katika mkutanojijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Liu Dong (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani jana katika ofisi za Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, kuhusu
manuafaa ya ujio wa Rais wa China, hali ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la awamu ya 12 pamoja na mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauri ya kisiasa
la awamu ya 12 la China. (kushoto) ni Mkalimaki kutoka Ubalozi wa China Jack Yu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini taarifa iliyotolewa na Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Liu Dong. (hayupo pichani) jana katika Ubalozi wa China nchini.
Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, LIU DONG (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam , baada ya kutoa taarifa kuhusu manufaa ya ujio wa ziara ya Rais mpya XI Jinping Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment