Mshambuliaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Thomas Ulimwengu, akichezewa vibaya na beki wa Morocco, wakati wa mchezo wa Kundi C wa Kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Mchezo huo umechezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa, ambapo timu ya Taifa Stars, imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku bao la kwanza likifungwa na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46, na mabao 2 yakifungwa na Mbwana Samatta katika dakika ya 67 na 80.
Ulimwengu akiendelea kuwahenyesha mabeki wa Morocco......

''Leo Mtanijua tu'', Ni Thomas Ulimwengu akionyesha uwezo mbele ya beki wa Morocco.....
beki wa Morocco, akikalishwa....

Beki wa Morocco, ajitahidi kutumia njia mbadala ya kumzuia Ulimwengu.....
''Heri Lawama Kuliko Fedheha bwana'', Beki wa Morocco akikubali yaishe kwa kumshika jezi Ulimwengu, laini wapi bado jamaa alikuwa na nguvu kama Faru na kumtoka na kisha kupiga krosi iliyowekwa nyavuni na Samatta.
Samatta (kushoto) na Ulimwengu, wakishangilia baada ya kutupia...
Mbwana Samatta, akimnyanyasa beki wa Morocco...
Wachezaji wa Stars, wakishangilia bao la pili....
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu ya Taifa....
Mrisho Ngasa, akimfinya Beki wa Morocco....
Shomari Kapombe, akiwekwa mtu kati na mabeki wa Morocco.
TIMU ya Taifa "Taifa Stars" leo imeweza kuwaduawaza Morocco baada ya kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Washambuliaji machachari wanaocheza soka la kulipwa katika Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, walidhihirisha umuhimu wao kwa timu ya taifa baada ya wao kung'ara kwa kutupia mabao hayo.
Bao la kwanza lilifugwa na Thomas Ulimwengu, Dakika ya 46 akitokea benchi baada ya kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto na mabao mawili yakifungwa na Mbwana Samatta.
Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C ikiwa na jumla ya pointi sita, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza ikiwa na pointi saba, baada ya jana kushinda jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Gambia.
Baada ya Ulimwengu kuingia, alionekana kubadili sura ya mchezo huku akigusa nyasi za uwanja huo na kurushiwa mpira na beki wake Erasto Nyoni, ambapo mpira huo ndiyo uliwekwa kimiani na mchezaji huyo, akiwa ameugusa kwa mara ya kwanza mara tu baada ya kuingia.
Bao hilo liliongeza kasi ya mchezo kwa upande wa Stars na katika dakika ya 67, Samatta aliifungia Satrs bao la pili akimchambua kipa wa Morocco, Nadir Lamyaghri, baada ya kupokea pasi ya Ulimwengu na kuifanya Morocco kuchanganyikiwa baada ya bao la pili na kuruhusu Stars kutawala zaidi mchezo.
Stars walionekana kuutawala mchezo huo huku wakionekana kupiga pasi nyingi zaidi na kukufua matumaini ya mashabiki wa Soka wa Nchini na waliofurika uwanjani hapo kuwashuhudia.
Dakika ya 80, alikikuwa ni Ulimwengu tena aliyemzidi nguvu beki wa Morocco, na kupiga krosi, iliyomkuta tena Samatta na kuifungia bao la tatu.
Beki Abderrahim Achchakir alipewa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi wa mchezo huo .
Kosa kidogo la safu ya ulinzi liliipa nafasi Morocco kupata bao lililofungwa na Yousef Elarabi aliyetokea benchi.











No comments:
Post a Comment