Habari za Punde

*KINANA ATUA BEIJING, ALAKIWA NA MARMO

  Balozi wa Tanzania Nchini China, Philip Marmo akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China, baada ya kuwasili leo Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
  "KARIBU BEIJING", Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, baada ya Kinana na ujumbe wake kuwasili akitokea jimbo la Sichuani, leo Machi 17, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini china kwa ziara ya siku kumi ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China.
 Baadhi ya Watanzania waliopo jijini Beijing, China wakichangamkia kupigapicha na Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (Katikati) nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing, wakilaki Kinana na msafara wake, nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing China, leo Machi 17, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing, Daninga .Daniel. Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.