Habari za Punde

*AZAM FC YAENDELEZA UBABE YAICHAPA NYUMBANI BYC II MABAO 2-1

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania timu ya Azam Fc, leo tena imeendelea kufanya vizuri katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya BYC II ya Lyberia, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa ATS, Jijini Monrovia. Mchezo huo ni wa kwanza ambapo Azam imejiweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika mchezo wake wa marudiano unaotarajia kupigwa hapa nyumbani hivi karibuni. Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Azam ilikuwa tayari imelala kwa bao 1-0, ambapo bao la kusawazisha na la kuongoza yalipatikana katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.