Habari za Punde

*KIPA MAHIRI WA TP MAZEMBE NA WENZAKE WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA GARI KINSHASA

WACHEZAJI watatu wa klabu ya DC Motema pembe-DCMP ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wamefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Kinshasa jana. 
Wachezaji hao ambao ni golikipa Guelor Dibulana, washambuliaji Hugues Muyenge na Mozart Mwanza walikuwa wakirejea kutoka katika Ibada maalum ya Ijumaa Kuu kuelekea Pasaka, iliyofanyika katika kanisa la Saint- Dominique lililopo Kinshasa.
 Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari lao walilokuwamo kugongwa na Lori. 
Kwa mujibu wa taarifa za hospitali mchezaji mwenzao Mbindi ambaye alikuwa akiendesha gari hilo alisalimika pamoja na abiria mwingine huku wao wakiwa wamepata majeraha makubwa. 
DCMP ilitarajiwa kucheza na timu ya  AS Vita Club leo jumalipi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.