Habari za Punde

*SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea zawadi kutoka kwa Mtoto  Hinaina Said Khalfan,wakati wa sherehe za siku ya Mtoto yatima zilizofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel  leo Mjini Zanzibar,shirika la misaada la I.H.H la Uturuki,kwa Ushirikiano na jumuiya ya Muzdalifa ya hapa Zanzibar kwa pamoja wamefanikisha kufanyika kwa sherehe hizo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti Muzdalifa,Sheikh Abdalla Hadhal, alipoangalia maonesho ya picha   mbali mbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Yatima katika Ukumbi wa Salama Bwawani leo, maadhimisho hayo yamefanywa na Shirika la I.H.H la nchini Uturuki kwa ushirikiano na Jumuiya ya Muzidalifa ya hapa Zanzibar inayoshuhulika kna Mayatima
Baadhi ya Wazee na Wanajumuiya ya Muzdalifa wallipohudhuria katika sherehe ya Siku ya Mtoto wa Yatima,katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar, wakisikiliza kwa makini Hotuba ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa katika hafla hiyo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.