Imeelezwa kuwa hadi sasa idadi kamili ya watu waliopatikana wakiwa wamekufa kwa kufukiwa na kifusi cha mabaki ya Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka jana kuwa imefikia 20, na miili yote ikifikishwa katika Hospitali ya Muhimbili, ambako shughuli ya kutambua miili ya marehemu ilikuwa ikiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo hadi saa tano leo asubuhi tayari miili mitani (5) ilikuwa imeshatambuliwa na ndugu zao.
Akizungumza katima mahojiano na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema kuwa hadi sasa tayari watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano, ambapo pia huenda na Ghorofa hili pichani lililo pembeni mwa ghorofa lililoporomoja nalo pia likavunjwa baada ya kujiridhisha kuwa halina ubora na viwango vinavyotakiwa.

No comments:
Post a Comment