Kamishna
wa Idara ya Sera ya manunuzi ya Umma, kutoka
Wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kulia) akizungumza jambo na mjumbe wa
kamati ya sera ya manunuzi, Clemence
Tesha, wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka
jana jijini Dar es Salaam leo. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na
wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Emmanuel Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania akichangia mada kuhusu utendaji kazi
wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya
manunuzi ya umma lililofanyoka jana jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo
la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma
kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi
binafsi.
Juma Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania
akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa
kutumia taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera
ya manunuzi ya umma.
Mkurugenzi wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Kamishna wa Idara
ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka Wizara ya Fedha Dk. Frederick
Mwakibinga (kushoto) akisalimiana na Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wakati wa
kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika
jana katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka
ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea kuhusu rasimu ya Sera ya manunuzi wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo
pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya
Umma lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati
wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma
lililofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini
Dar es Salaam.Picha zote na Anna Nkinda-MAELEZO








No comments:
Post a Comment