Habari za Punde

*MSANII KAJALA MASANJA ALIPONUSURIKA KWENDA JELA MIAKA SABA JANA, ALIPIWA FAINI YA SH. M 13 NA WEMA SEPETU

MSANII maarufu nchini, Wema Sepetu, amemnusuru msanii mwenzake Kajala Masanja, kwenda jela miaka saba baada ya kumlipia faini ya fedha taslimu ya Sh.milioni 13, baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili jana .
Hata hivyo wakati Kajala akiachiwa huru, mumewe Faraja  Chambo amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh milioni 213.

Wawili hao walitolewa hukumu ya kesi yao jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ya kula njama, kuuza nyumba iliyopatikana katika mazingira ya rushwa ili kuficha ukweli na kosa la 

utakatishaji fedha.


Mahakama ya Kisutu ilitawaliwa na vilio wakati hukumu ikisomwa, Kajala alikuwa akilia muda wote hali iliyosababisha na wasanii wengi waliofurika mahakamani hapo kuangua vilio kwa kububujikwa na machozi kwani hawakuweza kutoa sauti wakihofia kukamatwa kwa kuisumbua mahakama.

Hakimu Fimbo, alipomaliza kusoma hukumu Kajala alijikuta akikaa chini na kulia kwa huzuni, alitolewa nje kuelekea mahabusu na kuwaacha wasanii wakilia na kupanga jinsi ya kumsaidia aweze kutoka gerezani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.