Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na kulia ni Brigedia Hashimu Mbita.
Baadhi wa wadau wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.
Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
*******************************************
NA: FRANK SHIJA & BENEDICT LIWENGA- MAELEZO
VIONGOZI wahimizwa MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwataka viongozi nchini kukienzi na kuthamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.
Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mzee Kingunge ambaye alikuwa mgeni ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam .
“Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.
Aidha Mzee Kingunge anawaasa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali mfano Bungeni.
Hata hivyo, aliunga mkono lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.
Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata alama 90 hadi 95,lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.
“Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimua ya Chuo Kikuu,”alisema. Huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.
Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo Profesa Mugyabuso Mulokozi na Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi fasihi za Watanzania.
No comments:
Post a Comment