Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akizindua kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisi ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.
Naibu Balozi wa Uingereza nchini Julian Chandler akielezea jinsi nchi yake ilivyoona umuhimu wa kuandaa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akifuatiwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu Sarah Mount akielezea umuhimu wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Bernadeta Gambishi.

Wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisiya ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment