Wasanii wa Tanzania, Joseph Haule ‘Prof. J’ na Nice Mkenda ‘Mr Nice' ni miongoni mwa wasanii wa Afrika Mashariki ambao wamealikwa kupamba tamasha la badilisha live linalotarajia kufanyika nchini Uganda, April 26, makwa huu katika Viwanja vya Rugby Kyadondo.
Tamasha hilo la burudani linalotarajia kuwa kubwa zaidi kati ya matamasha yaliyowahi kufanyika nchini humo, linaratibiwa na Mwanamuziki wa Bongo Fleva wa nchini humo Dk. Jose Chameleone.
Akizungumzia Tamasha hilo, katika ukurasa wake wa Facebook, Chameleone, alisema kuwa, mambo yanaendelea kukamilika na Wasanii kibao walioalikwa tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.
Mbali na Prof. J na Mr Nice kutoka Tanzania, wengine ni Redsan kutoka Kenya na Massamba wa nchini Rwanda.

No comments:
Post a Comment