Habari za Punde

*WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA UCHUKUZI WATEMEBELEA RELI ILIYOHARIBIKA KWA MVUA DAR JUZI NA JANA TABATA MWANANCHI

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Uchukuzi ya namna RAHCO ilivyojipanga kuboresha njia za reli katika eneo lililoathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar. Wajumbe hao walifanya ziara hiyo leo mchana walipotembelea eneo hilo kujionea namna mvua zilivyoathiri Njia za Reli ya USafiri wa Treni Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akitoa maelekezo kwa Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania(TRL) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), wakati wa Ziara iliyofanywa na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi katika eneo la Reli lililoharibiwa na mvua leo mchana.
 Sehemu ya uharibifu uliotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. 
 Moja kati ya maeneo yaliliyoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.