Habari za Punde

*TAIFA STARS YAICHAPA MOROCCO 3-1 BILA JUA

Kikosi cha timu ya Taifa Stars. Timu hiyo leo imeonyesha maajabu na kuwashangaza waarabu wa Morocco, kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Awali Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF lilipanga mchezo huo uanze saa tisa kamili ili kuwawezesha wachezaji wa Stars waweze kufanya vizuri kutokana na wao kulizoea zaidi jua na joto kali, ambapo walihisi kuwa huenda waarabu hao wangeweza wasingeweza kucheza katika hali ya joto kali kutokana na kwamba wao wamezoea hali ya ubaridi. Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa mvua ilianza kunyesha kuanzia leo asubuhi na kuzua hofu kubwa kwa baadhi ya mashabiki wa soka waliokuwa wameamini taratibu hiyo iliyokuwa imepangwa na TFF jambo ambalo limewashangaza wengi baada ya Stars kuibuka na ushindi wa mabao hayo 3-1 huku kukiwa na hali ya hewa ya kawaida. HABARI KAMILI NA PICHA ITAWAJIA BAADAYE KAA NA UKURASA HUU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.