Habari za Punde

*BARRACK YOUNG YA LIBERIA YATUA DAR NA MATUMAINI KIBAO YA KULIPA KISASI KWA AZAM FC

Wachezaji wa timu ya Barack Young Controllers ya Liberia wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo, asubuhi tayari kwa mchezo wao wa marudiano na timu ya Azam Fc wa Kombe la Shirikisho, unaotarajia kuchezwa siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Picha na Habari Mseto Blog
Wachezaji hao wakiingia kwenye mabasi kuelekea Hotelini.
************************************

TIMU ya Barrack Young Controllers II ya Liberia imewasili jijini Dar es Salaam, leo asubuhi huku ikiwa na matumaini kibao ya kulipa kisasi cha kufungwa nyumbani kwao na wapinzani wao Azam FC.

 Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa timu hiyo, Robert Lartey, baada ya kuwasili amejigamba kuwa timu yake inauwezo wa kuifunga Azam FC kwenye mchezo wa marudiano wa  kombe la Shirikisho na hasa baada ya kurekebisha makosa yaliyoigharimu timu hiyo katika mchezo wa kwanza.

 “Mchezo huu ni muhimu kwa timu yangu na naamini nitashinda”, alisema Lartey.

Pia alijigamba kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji ambao pia wapo timu ya taifa ya Liberia ya Vijana, akina Ezekiel Doe, Benjamin Gbamy na George Dauda.

Aidha Kocha huyo amesema hali ya hewa ya Dar es salaam haijatofautiana sana na hali ya hewa ya Liberia, ambapo amesema kuwa Dar es Salaam kuwa na joto zaidi kidogo na Monrovia.

Msafara wa timu hiyo umetuwa na  watu 37,  wachezaji 21 na unaongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert Alvin Sirleaf, ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, Samuel Sumo wakati Meneja wa timu hiyo ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.

 Wachezaji waliotua na kikosi hicho ni Abraham Andrew, Alfred Hargraves, Alpha Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu Wee, Ezekiel Doe, George Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo, Joseph Broh, Junior Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince Kennedy, Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.