
Msanii chipukizi wa Muziki wa Injili nchini, Eveline Kabwelile, anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza ya muziki wa Injili inayokwenda kwa jina la 'YESU KOMANDO'.
Albam hiyo yenye jumla ya nyimbo tisa ameirekodia katika studio za Iki Production chini ya mwandaaji Iki.
Alizitaja nyimbo zilizomo kwenye alba hiyo kuwa ni:-
1. Yesu komando
2. Ananitosha bwana
3. Mungu hawezi kukusahau
4. Nakupenda mokozi
5. Mshukuru Mungu
6. Ni wewe mwenyewe
7. Usinipite Mokozi
8. Mokozi asifiwe
9. Ni nani
Albamu hiyo inatarajia kuzinduliwa Mei 12 mwaka huu, katika Kanisa la Hollyness pentecote kwa Mchungaji Ndalima Ubungo kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.
Akizungumzia sababu hasa iliyomfanya kuingia kwenye uimbaji wa Nyimbo za injili Eveline, amesema kwa upande wake anasukumwa sana na wito wa Mungu kwa kuwa alianza kupenda fani ya kuimba toka akiwa mdogo na kuona kuwa fani hiyo iko kwenye damu.
“Nilianza kuimba toka nikiwa mdogo sikumbuki ni mwaka gani, albamu hii nimeanza akuiandaa 2010 na 2011 ndio nikaanza kurekodi audio za nyimbo zangu na nilianza kurekodi video za nyimbo zangu mwaka 2012 katika studio Brayanz work chini Byayan Hasani na nyimbo zote zimeshakamilika audio na video tayari kwa uzinduzi”
Albamu ya audio na video ya albamu Yesu Komando itaanza kuuzwa siku ya uzinduzi

No comments:
Post a Comment