Habari za Punde

*KIKOSI CHA KWANZA CHA YANGA KINACHOANZA KUWAKABILI MAAFANDE WA ORJOLO


KIKOSI CHA YANGA Golini, anaanza Ally Mustapher, Shavu la kulia ni Juma Abdul, Shavu la kushoto ni David Luhende, Katikati ni Kelvin Yondani na Nadir Haroub 'Canavaro'.

Kiungo wa chini ni Athuman Idd 'Chuji' Kiungo wa juu ni Frank Domayo, Winga ya (kulia) ni Simon Msuva, Winga ya (kushoto) ni Haruna Niyonzima Mastraika ni Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu.

Wachezaji wa akiba ni:- Yusuph Abdul, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Salum Telela, Nurdin Bakari, Nizar Khalfan na Said Bahanuzi.

KIKOSI CHA JKT Orjolo, Golini ni:- Lucheke Mussa, Yusuph Machogoti, Majaliwa Sadiki, Nurdin Mohamed, Shaibu Nayopa, Salim Mbonde, Karage Mgunda, Emmanuel Memba, Paul Nonga, Idd Swaleh na Hamis Saleh.

Wachezaji wa akiba ni:- Shaibu Issa, Beno Alfred, Napho Zuberi, Markus Raphael, Sixbert Mohamed, Jackson Kamwela na Paul Malipesa.

 Timu ya JKT Orjolo leo inaingia uwanjani ikiwa na hamu ya kulipa kisasi cha mbao 1-0 iliyofungwa na Yanga katika mzunguko wa kwanza,mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwaka jana.

Na kwa upande wa Yanga leo inaingia uwanjani ikiwa na lengo moja tu la kutafuta Pointi tatu muhimu kwa kuhakikisha inaibuka na ushindi wa aina yeyote na kuendeleza ubabe kwa timu hiyo ya maafande na kuendelea kujiimarisha kileleni na kuongeza utofauti wa Pointi kati yao na Azam Fc ambayo kwa sasa ina Pointi 46 huku Yanga ikiwa na Pointi 49.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.