Habari za Punde

*MASHABIKI WA YANGA WAJIPANGA KUISHANGILIA SIMBA LEO IKICHEZA NA AZAM FC

KWA mara ya kwanza tangu kuanzishwa timu mbili zenye upinzani wa jadi za Yanga na Simba, ambazo pia hata mashabiki wake wanaupinzani wa kweli na wa jadi katika hata michezo ya kimataifa, leo mashabiki wa Klabu ya Yanga wamejipanga kuishangilia timu ya Simba kwa nguvu zote ili kuisapoti kuwafunga Azam Fc.

Hii inawezekana ni kutokana na upinzani wao wa jadi kwa kuona watani wao wakizidi kupotea na nafasi yao ikitishiwa kuchukuliwa na timu ambayo haina hata miaka kumi tangu ilipoanzishwa.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa mashabiki wa timu hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Baba Gire, alisema kuwa leo wameamua kuwasapoti watani wao wa jadi kutokana na kile wachokiona kwa  timu ya Azam kuonekana kujipanga na mizengwe ya kupanga matokeo ya mechi zilizobaki za Ligi Kuu.

Aidha alisema kuwa kutokana na kuona kuwa kumekuwa na tetesi za timu hiyo kutumia 'mlungula' ili kupanga matokeo katika mechi zilozobaki, kwa pamoja mashabiki wote wamemua kujitolea kuwashangilia Simba kwa moyo mmoja.

''Kiukweli tumejipanga kuwashangilia Simba kwa nguvu zote na kamwe hatuwezi kuwashangilia azam kwa hali halisi ya nafasi za timu zetu katika msimamo wa Ligi hii inayoelekea ukingoni, ila nao Simba wasituyeyushe wajitahidi kukaza angalau watupe moyo na nguvu za kuzidi kuwasapoti leo ili waone maajabu na kuwa tunawapenda watani zetu hatupendi wapotee''. alisema Baba Gire.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.