
*Asema ni mkakati wa Chadema kuua kes ya Lwakatare wao
*Mmwenyekiti wa Chadema Kata ya na wenzake 68 wahamia CCM
*Wadai Chadema imekubuhu kwa utapeli
*
NA BASHIR NKOROMO, GAIRO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni
na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.
Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
" Mambo haya yanayofanywa na wabunge kama ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio la jana ni aibu ya mwaka", alisema Nape.
Alisema, muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima busara na uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza malengo yao binafsi ya vyama vyao.
"Hatua hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho tosha". alisema Nape.
Alisema, hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.
"Haya ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba huu ni mkakati malum wa Chadema", alisema Nape
Mbali na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama.
"Inashangaza sana, Lisu badala ya kutoa ushahidi wake maghakamani kuhusu suala hili anakwenda kujzungumza na wandishi wa habari ili hali anafahamu wazi kwamba kesi kuhusiana na suala hilo ipi mahakamani, tafsiri yake ni kwamba ni juhufdi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama au kushawishi mahakama kutupilia mbali kesi kwa kigezo kwamna imeingiliwa uhuru wake", alisema na kuongeza:.
"Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe) pia wakati akizungumza Bungeni alitumia muda mrefu kuzungumzia suala la Lwakatare lililopo mahakamani. leo mahakama ionekane uhuru wake umeingiliwa iitupe kesi, na hata wakati wa kuchangia bajeti ya Utumishi, upande wa Chadema badala ya kuzungumzia sekta ya utumishi wa umma kurasa nne nzima zilihusu mambo ya Lwakatare", huu ni mkakati mbaya sana unaolenga haki isitendeke kuhusu kesi hiyo.
Akizungumzia hatua ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutamka bungeni kwamba CCM Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete na Chama Chake cha CCM ndiyo chanzo cha udini, aling'aka kwamba ni kauli inayotia shaka uelewa wa mambo wa mbunge huyo.
"Nina mashaka kama Lema ni mzima kiakili, CCM italetaje udini wakati ndiyo imeleta umoja na mshikamano kwa makabila zaidi ya 24 ya Tanzania kiasi kwamba amani na utulivu vimeshamiri? Yaani CCM ihangaike kujenga mshikamano halafu hiyo hiyo ione kicefuchefu kuilinda na kuanza kuihujumu? huu ni upuuzi wa hali ya juu sana", alisema Nape.
Nape alisema, vituko vyote vinavyoendelezwa na Chadema Bungeni na kwingineko ni dalili tisha kwamba wanaendelea kutekeleza ahadi waliyotangaza siku nyingi kwamba nchi haitatawalika.
Mkutano huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana inayoendelea mkoani Morogoro, ambapo pamoja na Nape, Kinana anafuatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib. Ni ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani humo.
WANACHAMA 68 WA CHADEMA WATIMKIA CCM Soma zaidi bofya chini
WANACHAMA 68 WA CHADEMA WATIMKIA CCM Soma zaidi bofya chini
TSUNAMI ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA taaban wilayani Gairo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama wilayani hapa, Zefania Magiga na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara, jana, Aprili 18, 2013.
Magiga na wenzake walikabidhi kadi zao za Chadema kwa Kinana, na kupewa kadi za CCM, baada ya kutangaza kukihama chama chao na kujiunga na CCM kwenye mkutano huo ambao ulifurika mamia ya wananchi, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Gairo B, katika wilaya mpya ya Gairo.
Mbali na kupokea wanachama hao kutoka Chadema, kwenye mkutano huo, Kinana alipokea wanachama wapya 120, waliojunga na CCM na kufanya jumla ya wanachama wapya waliojinga na CCM kwenye mkutano huo kuwa 188.
"Ndugu wana Gairo wenzangu na Watanzania wote, mimi kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Kata, nilikuwa naongoza wanachama wengi wa Chadema, na nilikuwa si mtu mdogo, lakini kwa muda ambao nimekuwa ndani ya chama hicho nimebaini kuwa viongozi wake wa kitaifa ni matapeli wa hali ya juu, ndiyo maana mimi na wenzangu tumeamua kuhamia CCM", alisema Magiga.
Alisema, akiwa Chadema alikuwa akishangaa kuona kwamba kila agizo alilokuwa akipokea kutoka viongozi hao wa chama hicho lilikuwa na kumwagiza kushawishi wananchi shari na kukataa kutii sheria za nchi, jambo ambalo alisema kwa muda mrefu akikuwa hakubaliano nalo kwa kuwa ni tofauti na lengo lililokuwa limemwingiza Chadema tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 15 iliyopita.
"Kwa kuwa sasa nnimeamua kurejea rasmi CCM, na hawa wenzangu (67) nimewaelimisha kwamba Chadema ni chama hatari nao wakanielewa sasa leo tunahamia wote CCM tunaomba mtupokee bila kinyongo, maana kufanya kosa si kosa kosa ni kulirudia", alisema Magiga baada ya kukabidhiwa kadi yake ya CCM na Kinana.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, alisema, uoamuzi wa wananchi wanaojiunga na CCM sasa na hata baadaye ni wa busara sana kwa sababu CCM ndicho chama ambacho bado cha kuaminika kwa malengo na matarajio yote ya maendeleo, amani na usalama wa Watanzania.
Kinana aliwataka wananchi wa Gairo na Tanzania kwa jumla kuendelea kuiunga mkono CCM ili iendelee kuwatumikia kwa kuwa bado ni chama imara kutokana na kuasisiwa katika misingi ya uhakika.
Mapema kabla ya mkutano huo, Kinana alifika katika kata mbalimbali wilayani Gairo na kufungua mashina ya Wajasiriamali wakereketwa wa CCM, ambapo pamoja na kuyafungua aliwahimiza kushina hayo kama kicocheo cha kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi wao na wa taifa.
"Tunapofungua mashina haya hatukusudii kuwa vijiwe vya kupigia soga tu, bali tunawataka wanachama wetu wa CCM myatumie kukaa pamoja na kuunda vikundi vya ushirika na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ambazo zinawatoa kwenye kulalamika kwamba hakuna ajira kwa kuwa mtakuwa tayari mnazo shughuli za kufanya", alisema Kinana.
Kinana alifungua zaidi ya mashina saba, abayo aliawaahidi wanachama wake kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuwasaidia kuinuka kiuchumi ambapo baadhi aliahidi kuwapa fedha au vitendea kazi kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza shughuli zao za maendeleo.
No comments:
Post a Comment