Habari za Punde

*RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME MKOANI DODOMA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Miundombinu ya kusambaza Umeme mkoa wa Dodoma, chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani (wa pili kulia) ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Daniel Wolde Johannes na (kulia) ni Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lendhardt wakimpongeza.Uzinduzi huo umefanyika leo katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na  Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lendhardt wakishuhudia uzinduzi huo wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizunguimza machache kuwasalimia wananchi kabla ya Rais kuzungumza.

 Rais Jakaya Kikwete, akisoma hotuba yake ya uzinduzi huo mbele ya wananchi waliofika kumsikiliza.
 Rais Kikwete, akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Daniel Wolde Johannes na (kulia) ni Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lendhardt (katikati yao) ni Makamu wa Rais Dk. Bilal.
 Rais Jakaya Kikwete, akiagana na wananchi wa kijiji hicho wakati akiondoka eneo hilo baada ya uzinduzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes katika picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.