Habari za Punde

*SIMBA YASINDIKIZA UBINGWA WA YANGA BAADA YA KUDROO 2-2 NA AZAM FC

 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Azam Fc, David Mwantika, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.
 Haruna Chanongo (katikati) akianguka baada ya kuwaramba chenga mabeki wa Azam Fc na kukwatuliwa karibu kabisa na eneo la hatari. Zaidi Bofya HAPA chini

 Haruna Chanongo, akijiandaa kupiga shuti.
 Mwinyi Kazimoto (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam Fc, wakati wa mchezo huo.
 Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba (kulia) akimtoka beki wa Azam Fc, Himid Mao, wakati wa mchezo huo.
 Kocha Msaidizi wa Simba, Julio (kulia) akimlalamikia Kamisaa wa mchezo huo, baada ya kuona mwamuzi wa mchezo huo, Oden Mbaga, akichezesha ndivyo sivyo.
Mafadha wa Simba wakiwa kwenye Benchi huku vijana wakiwajibika uwanjani wakati wa mechi hiyo.
***********************************************
MABAO mawili ya Simba katika mchezo wao dhidi ya Azam FC uliomalizika 
kwa sare ya mabao 2-2 imeipalilia ubingwa kwa Yanga kwa kuisimamisha 
Azam ambao walikuwa wanatishia ubingwa huo.

Matokeo hayo ni faida kwa Yanga ambayo kwa sasa inahitaji pointi sita 
(kwa kutegemea matokeo ya Azam FC) ili itangaze ubingwa kwani ikishinda 
michezo hiyo itafikisha pointi 58 ambazo haitafikiwa timu yoyote katika 
ligi hiyo.  

Azam sasa wamebaki katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 huku Simba 
wakiwa wamefikisha pointi 36.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika 
dakika ya 12 mfungaji akiwa Ramadhani Singano aliyemalizia kazi nzuri 
iliyofanywa na Mrisho Ngassa baada ya kuwatoka walinzi wawili wa Azam 
FC, Joakins Atudo na Lackson Kakolaki kabla ya kumtengenezea nafasi 
nzuri ya kufunga Ramadhan "Messi" Singano na kumchambua kipa wa wauza 
Ice Cream, Mwadini Ali Mwadini.

Bao hilo liliwachanganya wachezaji wa Azam FC na kuwapa mwanya 'watoto' 
wa Simba SC kutawala mchezo na kupachika bao la pili ya sita baadaye 
kufuatia ushirikiano kati yake na Haruna Chanongo na Ngassa tena kumtoka Kakolaki na kabla ya kumpa pasi safi Singano na kufunga kirahisi.

Kuona jahazi linakwenda mrama, kocha wa Azam FC ambaye awali alichezesha mabeki watano nyuma, alimtoa Kakolaki na nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha ambaye alibadili mchezo na kupata bao la 
kwanza dakika ya 29 kwa njia ya penati iliyofungwa kifundi na Kipre 
Tchetche.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kushambulia zaidi na huku 'watoto' wa Simba SC wakionekana kushindwa kuhimili vishindo na kuruhusa bao la kusawazisha katika dakika 71 kupitia kwa Humphrey Mieno kwa njia ya 'mkono' akimalizia mpira wa faulo wa Mcha.

Wachezaji wa Simba SC walimzonga mwamuzi Oden Mbaga wakilalamikia bao 
hilo na mwamuzi huyo  ambaye alionekana 'kupendelea' wapinzani wa Simba 
SC.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.