Habari za Punde

*WANAHABARI WAPEWA MAFUNZO KUHUSU RIPOTI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012

 Waandishi wa Habari wa  Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally (kushoto) na Mohamed Mohamed (kulia) wakisoma  ripoti ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu   wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. NBS iliandaa mafunzo hayo ya siku moja ili vyombo vya habari viweze kuripoti kwa usahihi taarifa ya sensa.
 Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Ephraim Kwesigabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kuripoti  kwa usahihi taarifa ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam.Zaidi Bofya HAPA chini

 Mratibu wa Sensa Zanzibar, Mayasa Mwinyi (kushoto) akimuelekeza mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Darlin Said (kulia) jinsi ya kutumia takwimu za sensa  ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala , matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
 Mchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka  ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ariv Severe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kutumia tovuti ya NBS ambayo inataarifa mbalimbali ikiwemo ya ripoti ya sensa  ya watu na Makazi ya mwaka 2012 wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyofanyika  leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
 Mwandishi wa Habari wa  Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Mohamed Ally  (kulia)  akiuliza swali wakati wa mafunzo ya siku moja ya waandishi wa habari yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam jinsi ya kutumia takwimu za Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu  yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) . Kushoto ni Mustapha Musa mwandishi wa habari kutoka Zenj FM.
Meneja wa Takwimu za watu na Jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Aldegunda Komba akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu uwiano wa idadi ya watu kijinsia  unavyotofautiana kimkoa kuanzia wanaume 88 kwa kila wanawake 100 kwa mkoa wa Njombe hadi wanaume 101 kwa kila wanawake 100 kwa mkoa wa Manyara. NBS iliandaa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo jijini Dar es ili vyombo vya habari viweze kuripoti kwa usahihi taarifa za sensa.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.