Habari za Punde

*MATUKIO YA PICHA KWENYE BONANZA LA WAANDISHI MEDIA DAY, MWAKYEMBE APIGA VIJEMBE, BLOGER FC YATISHIA TIMU ZOEFU

 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wanahabari wakati wa Bonanza maalum la waandishi wa habari 'Medi Day' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Katika Hotuba yake Dkt Mwakyembe, alisema ''Nataka Niwe Waziri Bora wa Uchukuzi Tanzania, Na pia wananchi hawataki Cheo cha Mtu bali wanataka Maendeleo zaidi, na hata yule anafanya kampeni wa Urais kwa wakati huu tukiwa na Rais, anavunja sheria za nchi, asubiri hadi tukifikia kipindi cha kampeni ndiyo aanze kujinadi''. alisema Dkt. Mwakyembe.
 Dj Sufianimafoto, akiwa na Mzee wa Full Shangwe, wakati wa kuwarusha watu kwa misebene na migoma ya mitambo ya SPM Sufiani Photo Magic, iliyokuwa ikisherehesha mahala hapo.
 Mashabiki wa timu ya Magazeti Tando, Bloger Fc, wakimbeba beki wa timu hiyo Sufianimafoto, wakishangilia naye baada ya kuwafungia penati muhimu ya mwisho iliyowapa ushindi dhidi ya timu ya DSJ, ambapo Bloger Fc ilishinda kwa mikwaji 3-2 na kuwaondosha mashindanoni, wapinzani. Zaidi Bofya HAPA chini

 Kipa wa Bloger Fc, Othman Michuzi, akibebwa juu na Father Kidevu baada ya kuokoa penati wakati wa hatua ya matuta na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi.
 Kikosi cha timu ya Blogers Fc katika picha ya pamoja na viongozi wao.
 Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo, wakishambulia wakati wakitoa shoo yao ya pamoja katika Bonanza hilo la waandishi, Medi Day.
 Father Kidevu akipagawishwa na sebene la Extra Bongo na kuamua kuingia kati kuanza kuyarudi masebene na wanenguaji wa bendi hiyo.
 Baadhi ya wasanii wa kundi la wachekeshaji la Comedi wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya sufianimafoto.
 Mzee Yusuph, akiimba mbele ya waandishi akiwapagawisha na kuwaacha hoi...
 Mpiga picha maarufu wa Habari Maelezo Mwanakombo Jumaa (katikati) akipozi na wenzake na Mzee Yusuph kwa picha.
 Mzee Yusuph akiimba jukwaani na kundi zima la Jahazi...
 Somoe Ng'tu na Zena Chande (kulia) wakisebeneka na miondoko ya mzee Yusuph....
 Mzee Yusuph akiimba na kucheza pamoja na wanahabari kati.....
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, akizungumza wakati wa Bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.