Habari za Punde

*YANGA YAVUTWA SHATI NA MGAMBO JKT YATOKA SARE YA BAO 1-1

Dakika 90 zimemalizika timu za Yanga ya Dar es Salaam, leo imevutwa shati na Mgambo JKT kwa kutoka sare ya bao 1-1.

Bao la Mgambo lilifungwa na Issa Kanduru katika dakika ya 43, kipindi cha kwanza na kufanya timu hizi kwenda mapumziko huku Mgambo ikiwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha pili, Simon Msuva aliisawazishia timu yake ya Yanga katika dakika ya 86 na kufanya timu hizo kutoka sare.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.