Habari za Punde

*ZIARA YA KINANA ULANGA MOROGORO AVUNA KADI KIBAO ZA CHADEMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga, alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent Edward.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro.
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano  mkubwa wa hadhara  uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye  Kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni  Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib. Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.