Habari za Punde

*ANGALIA AKILI YA DEREVA HUYU v/s MNYAMA HUYU

 Hapa ilikuwa ni barabara mpya inayotokea Bagamoyo kuelekea mikoa ya Kaskazini inayochomokea njia panda ya Chalinze, ambapo Mnyama huyu alikuwa akikatiza barabara kuelekea upande wa pili wa barabara hiyo, huku (kushoto) ni Lori lililokuwa katika mwendo na (kulia) mwa Lori hilo ilikuwa ni Coaster iliyokuwa ikijaribu kulipita Lori hilo.

Wakati Coaster ikikaribia kumaliza bodi ya Lori ndipo Mnyama huyu akatokea upande wa pili akivuka huku akikimbia kwa mbwembwe akiruka ruka jambo lililowafanya abiria waliokuwa katika Coaster kumfurahia huku wakimsikitikia  kuwa huenda asingewahi kuvuka kabla ya kulambwa tairi na Lori.

Lakini wakati abiria hao wakifurahishwa na Mnyama huyu ambaye alikuwa mithili ya Nyani, ghafla Dereva wa Lori aliwashangaza watu baada ya kutumia bodi kubwa ya Lori lake lililokuwa na tera 'Eti' kumkatia denge mnyama huyo ili amkanyage na ndipo Lori hilo liliyumba na kutaka kuanguka huku likitoka nje ya Barabara huku mnyama huyo akikatiza kiulaini na kuondoka zake.

Sasa sijui kama Dereva huyu angeangusha gari angejieleza alikuwa akifanya nini, au angeelezeaje sababu za kuangusha gari. MADEREVA, UTULIVU, AKILI NA BUSARA MUWAPO BARABARANI NDIYO KITU CHA KWANZA.
Hapa Lori hilo likitoka nje ya Barabara kumkatia denege mnyama huyo, ambapo lilimkosa na kuyumba wakati likijitahidi kurudi barabarani na kutaka kusababisha ajali kwa kuigonga Coaster iliyokuwa pembeni yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.