Habari za Punde

*BAADA YA RIPOTI YA SUFIANIMAFOTO HATIMAYE KITUO CHA POLISI KIMEFUNGULIWA, LAKINI HUDUMA JE???

"BAADA YA RIPOTI KAMILI YA SUFIANIMAFOTO, HATIMAYE KITUO HIKI SASA KIMEFUNGULIWA". Lakini pamoja na kufunguliwa kwa kituo hiki bado hakionyeshi kama kinafanya kazi ipasavyo kama ilivyokuwa kwa vituo vingine ilivyozoeleka. 

Picha ya chini ilipigwa majuzi na kuwekwa hewani na mtandao huu ikielezea jinsi kituo hiki kinavyokuwa kimefungwa muda wote na kunyimwa hadhi halisi kulingana na aliyekifungua kwa wakati huo, aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mhe. John Malecela, aliyekifungua tarehe 21/9/1991. 

Baada ya juzi tarehe 23,mwezi huu kuchapisha picha hii katika ukurasa wa mtandao huu, hatimaye leo kimefunguliwa kama ushahidi tu, Je wahusika waliopangiwa kazi katika kituo hiki wanaripo gani na je bosi wao anafahamu kuwa kituo hiki hakifanyi kazi na tangu kilipofunguliwa kilifanya kazi kwa muda gani na tatizo hasa ni nini hadi kufikia kufungwa siku hizi?
Hii ndiyo picha iliyopigwa majuzi wakati kikiwa kimefungwa na kufuli huku bango lake likionyesja kuwa ni Kituo cha Polisi Kata ya Viwandani, kilichopo barabara ya Singida mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.