HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA KIMELAZIMIKA KUVUNJIKA BAADA YA KUTOKEA MVUTANO WA KISHERIA BAINA YA WABUNGE WA UPINZANI NA KITI CHA SPIKA WA BUNGE.
WAKATI YAKITOKEA HAYO, MHE. SPIKA ALIMTAKA KIONGOZI WA UPINZANI KUKAA CHINI ILI KUMPISHA MREMA KUCHANGIA MUSWADA WA SHERIA WA KATIKA KATIBA MPYA, AMBAPO MHE. FREEMAN MBOWE ALIGOMA KUKAA CHINI, JAMBO LILILOMFANYA SPIKA JOB NDUGAE, KUWAALIKA ASKARI ILI KUMTOA NJE YA UKUMBI HUO FREEMAN MBOWE.
BAADA YA MBOWE KUTOLEWA NJE HUKU AKISINDIKIZWA NA ASKARI, WABUNE WOTE WA UPINZANI WALITOKA NJE NA KUFANYA KIKAO HICHO KUAHIRISHWA KWA MUDA.
No comments:
Post a Comment