Habari za Punde

*FULL MOVIE TOLEO JIPYA LA VITUKO VYA WABUNGE MJENGONI, MBILINY v/s POLISI NGUMI NJE NJE

Full Movie Toleo jipya la Wabunge Mjengoni
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa ameng'ang'ania  Microphone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa katika ukumbi wa Bungeni Mjini Dodoma jana. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI ENDELEA
Wabunge wa Upinzani wakimlinda Kiongozi wao, Freeman Mbowe, asitolewe ukumbini jana.
Ulinzi ukiendela....
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, akiendelea kung'ang'ania  Microphone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa ukumbini Bungeni Mjini Dodoma jana. Hata hivyo   Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafanikiwa kumtoa nje.
  Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafanikiwa kumtoa nje-
 ''Duuh Sasa hiki kituko, sijui hii Movie itazinduliwa lini wananchi wanunue wajionee wenyewe majumbani''. Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni.
Timbwili likiendelea....
 Mbunge  wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa  na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka ukumbini Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya  hivyo na Naibu Spika wa  Bunge, Job Ndugai.
Wabunge wa upinzani wakitoka nje.....
 Mbunge wa Mbeya Mjini  akizuiwa na wabunge  wa CHADEMA ili asiendelee kupambana na polisi, Bungeni Mjini Dodoma.
 Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini. 
 Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi.....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.