Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi Kikombe kwa kiongozi wa timu ya Wilaya ya Korogwe, hivi karibunu. Picha na Maktaba.
***********************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
TIMU ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais, inayojiandaa na mashindano ya SHIMIWI inayotarajia kuanza mwezi huu mkoani Dodoma, mwishoni mwa wiki ilitoka sare kwa kufungana bao 1-1 na timu ya Jumuiya ya ISTIQAAMA ya jijini Dar es Salaam, katika mchezo wao wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja Dar es Salaam Zoo uliopo Kigamboni.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia Mgeni rasmi alikuwa ni Katibu wa Makamu wa rais, Zahro Mohammed, ambapo vijana wa Ofisi ya Makamu wa Rais walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 47 kupitia mshamuliaji wake, Simon Kifaru, aliyeweza kuitendea haki pasi nzuri ya kiungo wake, Mandia.
Baada ya bao hilo, timu ya ISTIQAAMA, ilijipanga na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 79, kupitia mshambuliaji wake matata, Saleh Omar Saleh, aliyeunganisha krosi nzuri ya winga wake wa kushoto, Suleiman Omar, aliyetokea benchi.
Katika mchezo huo, Golikipa wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Jumanne Abdallah, alikuwa Nyota wa mchezo huo kutokana na umahiri wake wa kuokoa michomo na kuonyesha umahiri wa kudaivu na kuficha mipira ya hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwake.
Mashabiki waliohudhuria mchezo huo walipata burudani ya aina yake kutokana na umahiri wa wachezaji wa zamani waliokuwa wakionyesha vitu adimu vilivyokuikionyeshwa na beki kisiki wa OMR, Japhet ambaye alikua
akimdhibiti vilivyo mshambuliaji wa ISTIQAAMA, Saleh Omar.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kapteni wa timu ya OMR,
Mandia aliwashukuru wachezaji wa timu zote mbili kwa mchezo mzuri ambao ulikuwa ni sehemu ya kufahamiana na kudumisha udugu, na kuahidi
kujipanga vizuri kwa ajili ya marudiano.
Aidha Nahodha huyo alisema kuwa timu yake imetoka sare kutokana na kutokuwepo kwa wachezaji wake mahiri kama, Muhidin Sufiani, Masoud Balozi na Amour Nassor, waliokuwa na majukumu ya kikazi.

No comments:
Post a Comment