Habari za Punde

*WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA MAONYESHO YA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI CHINA

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini  China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne yana lengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo waweze kufanya biashara na watanzania. Kulia kwa waziri mkuu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na kushoto kwake ni Balozi wa China nchini LV Youqing.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia malighafi zinazotumiwa na  kampuni ya Beijing New Building Material kutengenezea nyumba alipotembelea banda hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza  kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa  wa Kampuni hiyo Alec Lu na wapili kulia ni Makamu Meneja Mkuu Fred Yu.
 Mfanyakazi wa kiwanda cha Changzhou Amec Group cha nchini China Yan Xing Long (kulia) akimueleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda jinsi mashine ya kuchanganya kokoto iliyotengenezwa na  kiwanda hicho  inavyofanya kazi  wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia mfano wa nyumba zinazojengwa na kampuni ya Beijing New Building Material alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wapili kulia  ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na watatu kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa  wa Kampuni Alec Lu.
Baadhi wa watu mbalimbali walioshiriki  ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China  yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne ambayo yamefunguliwa leo yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo yaweze  kufanya biashara na watanzania.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.