Habari za Punde

*URGENT HELP, WADAU UTAPELI HUU NI HADI NLINI?? JE NI KWELI NI BADI HUYU TUNAYEMJUA AU???

I'm Sorry for bothering you with my problem,I'm presently in England,something extremely Awful happened to me,I was robbed at gun point on my way to the Hotel by some Hoodlums and they made away with my Bag and other valuables.I would have called you but don't have a phone presently.I have reported to the police and they are investigating the matter but its taking a longer time and I want to get back home.I have spoken to the embassy here but they are not responding effectively to the matter. This is shameful,I need you to help me with a loan of 1,350 pounds to pay my hotel bills and get my self home.I will Pay you back with interest.I will appreciate whatever amount you can assist me with. Let me know asap.

My hopes on you
 
--------------
John Hans Badi
-Senior Photojournalist
-Director of Hans PR (Public Relations, Press Coordination, Photography, Videography & Promotion Activities).
-Blogger: Daily Mitikasi Blog
P.O. Box 11717, Dar es Salaam.
Mobile: +255784567088
E-mail:badijohn30@yahoo.co.uk
****************************************************
HUU ndiyo ujumbe nilioupata hivi punde kupitia Email yangu, kama rafiki wa karibu na mweny picha hiyo hapo juu, ambaye si mara moja huwa tukiwasiliana kwa email na simu, lakini cha kushangaza zaidi leo baada ya kupokea ujumbe huu, nimejaribu kumtafuta hewani, simu yake imepokelewa na Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Pendo, anayeishi Mkoani Arusha ambaye amedai kuwa namba hiyo na mali yake na anaitumia tangu mwaka 2000.

Aidha Mwanamke huyo ameshitushwa na simu yangu baada ya kumuuliza kuwa yeye ndiye mwenye simu hiyo??

''Samahani dada yangu, ni nashida na mwenye simu hiyo'', niliongea simuni huku nikijua kuwa huenda ameachiwa simu hiyo kwa muda ama katika chaji, lakini mdada huyo, alishuka na kusema.

''Jamani wewe kwa leo hii ni mtu wa tatu unanipigia na kuniulizia mtu huyo sijui Badi, ambaye mimi simjui na simu hii ni mali yangu nawaomba mwende Airtel na mkaulize mmiliki wa simu hii ni nani mtapata jibu, mimi ninaitumia simu hii tangu mwaka 2000'' alimaliza kusema na kujitambulisha kwa jina moja la Pendo.

Kwa maana hiyo basi inawezekana kuwa ujumbe huu haukutumwa kwangu tu bali umetumwa kwa rafiki wote wa karibu na Badi, ili kwa atakayelegea na kukurupuka basi aweze kumtumia mzigo fasta fasta.

Kwangu mimi ujumbe kama huu wala si wa kwanza kuupata ukielezea maswahiba yanayotungwa kuwa yamewapata rafiki zangu, na pia kibaya zaidi yalishanikuta mimi binafsi kwa kutumwa ujumbe kama huu ukielezea kuwa nimepatwa na tatizo nikiwa nchini Spain, nchi ambayo sijawahi hata kufika.

Nilichofanya baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya rafiki zangu walio nchini Uingereza, akiniuliza kuhusu tukio lenyewe, niliamua kubadili Passward ya email yangu na kuwatumia ujumbe rafiki zangu wote kuwajulisha kuwa ujumbe uliotumwa kwao kuhusu mimi si wa kweli na nilikuwa salama wala sikuwa nikihitaji msaada wa pesa zilizotajwa.

wengi walinielewa na kuwahi kunijibu, Sasa kwa hili rafiki yetu John Badi, tunamuomba na yeye pia atujulishe tena kwa lugha ya kinyumbani yaani KISWAHILI,  ili tuweze kujua, kwani kwa sasa hapatikani katika simu tuliyozoea kumpata, ambayo kwa sasa ukipiga anapokea mwanamke aitwaye Pendo wa Arusha.

Kwani Wabongo tumesha zoea tupatapo matatizo si rahisi kuanza kuumiza kichwa kuwatafuta rafikizo katika mitandao tena kwa kutumia lugha ngumu kuwahi kueleweka 'KIKRISTO' yaani Kiingereza wakati kuna lugha nzuri ya kunifanya nikuelewe mapema na kujua kuwa kwa lugha hii ni kweli rafiki yangu amepatwa na tatizo. 

TUWE MACHO JAMANI NA MITANDAO HII AMA MESEJI KAMA HIZI, KILA UPATAPO UJUMBE KAMA HUU USIKURUPUKE KUKIMBILIA ATM NA KUDROO MZIGO ILI KUMSAIDI RAFIKIYO UTAKUWA UKIWASAIDIA 'WASHENZI' FLANI TU NA BAADA YA MUDA UNAGONGANA NA RAFIKI YAKO HUYO PANDE ZA POSTA AKITOKWA NA JASHO JINGI KUTOKANA NA JOTO KALI LA bONGO, UNABAKI NA MSHANGAO NA HATA KUZIMIA KWA PRESHA YA MZIGO ULIOMTUMIA.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.