Habari za Punde

*BABU SEYA NA MWANAWE PAPII KOCHA WAWASILISHA SHAURI LA KUTOLEAA HUKUMU YA KESI YAO UPYA MAHAKAMA YA RUFAA LEO

 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii Kocha' wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa ya kesi yao kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na ulawiti. Picha na Francis Dande
 Baadi ya watu waliohudhuria kusikiliza rufaa hiyo leo katika mahakama ya Rufaa.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza au Papii.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.
 Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson  Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu iliyoitoa mwaka 2010.
 Johnson  Nguza 'Papii' akibusu mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani.
 Papii Kocha, akinyoosha mkono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa hatua waliyofikia juu ya Rufaa ya kesi yao.
 Picha ya chini najuu, Mpiga picha wa ITV, Magomeni namwenzake nao wakilamba ardhi baada ya kujikwaa katika harakati za kunasa tukio hilo.
Magomeni, bwana eti yeye chini, lakini kifaa cha kazi NOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.