
Mabadiliko hayo yamefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo leo imemteua Afisa Habari wa Shirikisho hilo, Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, uteuzi huo ukiwa umeanza rasmi kuanzia jana Novemba 2 mwaka huu.
Aidha baada ya uteuzi huo sasa Kamati hiyo imempa likizo yenye malipo aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah,ambaye ameagizwa kuwa aende likizo ya malipo hadi mkataba wake utakapomalizika rasmi.
Pia Kamati hiyo ya Utendaji imeviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote wa Soka nchini na waandishi wa habari, kumpa ushirikiano Kaimu huyo Katibu Mkuu wa TFF Boniface Wambura, katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi chote atakachokuwa akikaimu nafasi hiyo.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es Salaam
Novemba 3, 2013
No comments:
Post a Comment