Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu makubaliano ya kukabidhi mgodi wa Tulawaka kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutoka kwa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Afrikan Barrick Gold (ABG).
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),Gray Mwakalukwa (wa pili kushoto) na Makamu wa
Rais wa Afrikan Barrick Gold Mine, Deo
Mwanyika (wa pili kulia) wakitia saini leo makubaliano ya kukabidhi
mgodi wa Tulawaka kwa STAMICO. Kulia ni
Mshauri Mkuu wa Afrikan Barrick
Gold Mine Katrina White na Kushoto
Mkurugenzi wa Utafiti kutoka STAMICO Gideon Mwaya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Gray Mwakalukwa (kushoto) na Makamu wa Rais wa Afrikan Barrick Gold Mine, Deo Mwanyika (kulia wa pili )wapeana mikono baada ya kutia saini leo makubaliano ya kukabidhi mgodi wa Tulawaka kwa STAMICO. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Afrikan Barrick Gold Mine Katrina White. Picha na na Magreth Kinabo –Maelezo
No comments:
Post a Comment