Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Ali Mbaruk akieleza kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu michezo mbalimbali itakayofanyika ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayo adhimishwa Mwezi
January 2014,wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
Leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Assah Mwambene.
**********************************
Frank Mvungi -
Maelezo
Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeandaa mashindano ya michezo 17 kuadhimisha miaka 50
ya mapinduzi hayo itakayofikia kilele januari 12,2014 ambayo ni siku ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa
na Waziri wa Habari , Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Mh. Said Ali mbaruk wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua
iliyofikiwa katika maandalizi ya michezo ya kuadhimisha mapinduzi hayo.
Mh. Said Ali Mbaruk amesema kuwa katika kuadhimisha mapinduzi hayo michezo
mbalimbali itafanyika ikiwemo mpira wa miguu, riadha, volleyball, Table tenis na
mazoezi ya viungo.
Akifafanua
zaidi Alisema michezo hiyo pia
itawahusisha watu wenye ulemavu ambapo kwa kushirikiana na Kamisheni ya utalii
michezo mingine itakayofanyika ni karata,bao,squash
na kuogelea .
Akieleza
zaidi Mh. Said Ali Mbaruk aisema kuwa
katika michezo hiyo kutakuwa na timu zaZanziba,Tanzania bara,Afrika
Mashariki,ambapo mashindano hayo yanapata hadhi ya kimataifa.
Pia alizitaja
timu zinazotarajiwa kushiriki kuwa ni Azam FC,Simba, Yanga,Mbeya city kwa
upande wa Tanzania bara, baadhi ya timu toka Zanzibar ni chuoni,Pemba combine
na Unguja combine.
Katika
maadhimisho hayo mechi zote zitatangazwa moja kwa moja kupitia ZBC TV,kwa kushirikiana
na Azam TV.
No comments:
Post a Comment