Habari za Punde

*MECHI YA 'MABOMU' YA SIMBA, KAGERA YAINGIZA SH. MILIONI 32

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera iliyochezwa jana (Oktoba 31 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mirindimo ya mabomu huku mashabiki wa Simba wakifanya vurugu na uharibifu wa kung'oa viti, imeingiza jumla ya sh. 32,726,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 81 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 5,541 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,992,101.69, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,183,890 wakati kila klabu ilipata sh. 7,242,252.45.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 3,682,501.25, gharama za mchezo sh. 2,209,500.75, Bodi ya Ligi sh. 2,209,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,104,750.37, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 859,250.29.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.