Habari za Punde

*MHE. ZITTO KABWE NA DKT KITILA MKUMBO KUKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KESHO KUTOA MSIMAMO WAO

Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo, kuwa watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho siku ya Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni. 
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa5.00 asubuhi.
Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Novemba 2013. 
Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.