Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzowe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
Sehemu ya umati wa Wananchi wa mjini Mbeya wakiushangilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ukupokuwa ukiwasili kwenye Viwanja vya Ruanda Nzowe, kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Baadhi yavijana waliohudhuria mkutano huo wakinasa matukio kwa kutumia simu zao za mkononi.
Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wenye shauku ya kumsikiliza, wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akihutubia maelfu ya wananchi wenye shauku ya kumsikiliza, wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya.
Katibu wa Chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM, akizungumza baada ya kupewa muda na kujitambulisha rasmi katika gwanda la Kijani.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi wenzake wakiwa kwenye meza kuu wakati wa mkutano huo. Meza kuu hiyo ilikuwa tofauti kabisa na zile zlizozoeleka ambazo huwa na mapambo mengi huku zikiwa na sehemu ya kukinga jua. Utaratibu wa majukwa na meza kuu vya aina hii ndiyo mtindo wa sasa katika mikutano ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na kijana Japhet Mwasele katika Bajaj wakati msafara wake ukienda kwenye mkutano wa hadhara aliofanyika jana kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe, mjini Mbeya, mwishoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye bajaj wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ukienda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Viwanja vya Ruanda Nzovwe, mjini Mbeya, mwishoni mwa ziara ya Katibu Mkuu huyo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua mkoani Mbeya.









No comments:
Post a Comment