Bondia wa ngumi za kulipwa Fadhili Awadh amefariki dunia katika hospital ya mwananyamala baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Fadhili Awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia waliochaguliwa kucheza pambano la ubingwa tarehe 29 mwezi huu dhidi ya mpinzani wake kutoka mkoani Tanga, Alan Kamote, ambapo alikuwa tayari ameshaanza maandalizi ya pambano hlo.
Imeelezwa kuwa sababu ya kifo chake kwa mujibu wa ripoti ya Daktari wa Hospitali ya Mwananyamala kwa kiongozi wa Ngumi Ibrahim Kamwe ni kuwa Fadhili, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadilika pale alipojaribu kufanya mazoezi na kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku mbili akiendelea na matibabu hadi umauti ulipomkuta.
Fadhili, mwenye umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabasaba, akiwasindikiza mabondia Japhet Kaseba na Thomas Mashali.
Sisi tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi ,Ailaze roho ya marehemu Fadhili Awadh “Tiger” peponi, Amina, shughuli za maazishi zinafanyika nyumbani kwao maeneo ya manzese.
No comments:
Post a Comment