Habari za Punde

*BREAKING NEEEWZZZ!!!! YALE YALEEEE, SITTA AHAIRISHA BUNGE

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mh Sammuel Sitta amelazimika kuahirisha kikao cha bunge hilo leo jioni baada ya kutokea kutoelewana baina ya wajumbe ambao walianza kuzomea kama ilivyo kawaida yao. Mtafaruku huo umezuka baada ya baadhi ya Wajumbe na Baadhi ya wabunge wa upinzani kupinga Jaji warioba asiwasilishe rasimu ya katiba leo badala take asubiri hadi Rais atakapokuwa amezindua rasmi bunge hilo jambo ambalo lilizua mtafaruku wa sintofahamu huku wengine wakitaka Warioba kuwasilisha Rasimu baada ya Mhe. Rais Kulihutubia bunge hilo kwanza. Mwenyekiti wa Bunge akaruhusu Jaji Warioba aendeleee na Uwasilishaji lakini wabunge wakaanza kujibizana na kupiga makofi na meza za bunge huku wakizomea na baadhi ya wajumbe wakitoka nje na wengine  wakisimama.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.