Habari za Punde

*MGIMWA NDIYE MBUNGE WA KALENGA, CHADEMA WAPINGA MATOKEO


Godfrey Mgimwa na Robby Mgimwa wakionesha hati yao ya ubunge baada ya kukabidhiwa leo, wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga uliofanyika jana. 

Mbunge mteule wa jimbo la Kalenga Bw Mgimwa akiwa na nyuso ya furaha baada ya kutangazwa mshindi, huku akionyesha dole alama ya CCM.

Msafara wa magari yakipita katika mitaa ya Kalenga kwa shangwe na nderemo baada ya kutangazwa matokeo.


Boda boda wakifanya yao katika kusherehesha ushindi huo.


CHADEMA WAPINGA MATOKEO YA KALENGA

Tendega akizungumza na wanahabari 
Akizungumza na wanahabari nje ya iliyokuwa kambi ya Chadema mjini Iringa ya CK Lodge, Tendega alianza kwa kumshukuru Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na viongozi wengine wote walioshiriki kampeni za chama hicho. 



Huku baadhi ya wafuasi wa chama hicho wakiangua kilio alisema; “Ninawashukuru makamanda wenzangu na wanaharakati waliokuwa wanapigania haki Kalenga, wafuasi na wanachama wa Chadema wote, nawapa pole na hongera kwa kuanza na kumaliza uchaguzi huu uliokuwa na dosari nyingi,” alisema. 



Alisema maapambano ya ukombozi yana changamoto nyingi na kwamba huo ni mwanzo wa safari ya mabadiliko makubwa nchini, pale walipokesea mbele ya safari watajipanga upya. 
Benson Kigaila.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.