**********************************************
Frank Mvungi-MAELEZO
IMEELEZWA kuwa
Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji
wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni 480 kwa mwaka.
Hayo yamesemwa
na Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi
kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka Wilayani Monduli mkoani Arusha.
Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira
zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana
na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.
Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya
uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.
Ngapemba alibainisha kuwa madini
ya magadi soda yanatumika viwandani
katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za
hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza
karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.
Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka
2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu
tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia
uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda.
Alisema kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata
ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.
“Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha
mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo
milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba na kuongeza:
Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii
mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika
hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
No comments:
Post a Comment