Habari za Punde

*VURUGU ZA WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

 Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo mchana baada ya Bunge hilo kuahirishwa ghafla kwa muda kutokana na kufuatia kutokea Sintofahamu baina ya wabunge waliokuwa wakirushiana maneno bila kujali utaratibu na kutishia kushikana mashati jambo lililomfanya mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Ameir Pandu Kificho kutangaza kuliahirisha kwa muda.
*******************************************************Na Augusta Mafoto, Dodoma
Katika hali ya isiyokuwa ya kawaida ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mchana kumeibuka mtafaruku baina ya wabunge na kuzua vurugu Kutokana na Vuruguru Kutokana na Hali ya Kutokuelewana kati ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mhe. Ole Sendeka, Kutoleana maneno na Mbunge Mwenzake wakati Mbunge Huyo alipohoji kuhusu Kanuni za kuendesha kikao hicho.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (watatu kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusiahirishwa kwa muda leo mchana baada ya kutokea vurugu baina ya wabunge waliotaka kushikana mashati. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.