Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya kujenga mwili na yahusuyo mchezo wa ngumi kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo huku akikutana na mabondia mbalimbali kupima uwezo wao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Chokoraa alisema kuwa hivi sasa amejiandaa kuwathibitishia mashabiki wake kuwa ana vipaji tofauti tofauti kikiwamo cha ngumi.
Chokoraa amekuwa akijifua katika Gym ya Bigright Boxing iliyopo Mwananyamala jijini Dar, chini ya mwalimu wake bondia mkongwe Omar Athuman ‘Van Dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake ambaye amekuwa akijitapa kumfanya Chokoraa, kuuchukia mchezo wa ngumi.
Pambano hilo litakuwa ni moja kati ya michezo ya utangulizi katika pambano la ubingwa wa UBO-Afrika kati ya Karama Nyilawila na Said Mbelwa.
Mapambano mengine ni kati ya Suleiman Galile akimkabili Abdallah Pazi, ‘kiroba’ Alan Kamote na Adam Ngange, Ramadhan Kumbele na Hassan Kiwale 'Morobest' , Idd Athuman na Julius Kisarawe, Zumba Kukwe wataoneshana kazi na Kamanda wa Makamanda.
Pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi kati ya mabondia wa Tanga watakaozipiga na mabondia wa Dare es salaam, kama vile Athuman Boxa wa Tanga atazipiga na Waite Juma wa Chalinze, Rajabu Mahoja wa Tanga atazipiga na Kaisi wa Dar.
No comments:
Post a Comment