Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA SHEREHE ZA KIJADI ZA WASUKUMA WILAWANI MAGU MKOA WA MWANZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhiwa Usinga na wazee wa kijiji cha kisesa wilayani Magu baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la wasukuma na, wakati wa Sherehe za kijadi na maadhimisho ya siku ya ngoma na nyimbo za kabila la kisukuma zilizofanyika Wilayani magu mkoani Mwanza, mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga  Ngoma  kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Ngoma na Nyimbo katika Maadhimisho ya Tamasha la Jadi la Wasukuma  kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, azungumza na Mtoto  Fredrik  Emmanuel  baada ya Kumalizika kwa Sherehe za Uzinduzi wa tamasha la Ngoma na Nyimbo za Kabila la wasukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha kisesa mkoani mwanza, Wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  alipokua akiwahutubia  kwenye Uzinduzi wa Mashindano ya Ngoma na Nyimbo za kabila la kisukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Ngoma ya Kabila la Wasukuma wakati wa Tamasha la siku ya Bulabo  zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilayani Magu Mkoa wa Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuagana na wananchi  wa kijiji cha kisesa baada ya kuzindua  Mashindano ya Ngoma na Nyimbo za kabila la Wasukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilayani  Magu Mkoni Mwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.