Habari za Punde

*HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA KWA UFUPI

DODOMA TANZANIA:- Jumla ya Vizimba 62 vya biashara, Vipodozi, Viatu  vyateketea kwa moto katika Soko la Sarafina lililopo Stendi ya Jamatini Mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Imethibitishwa na Mwenyekiti wa Soko hilo, P. Machela, haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha moto huo.

AJALI YA BASI YAUA CHINA:- Jumla ya watu 11 wamefariki dunia katika ajali ya basi dogo lililokuwa limebeba wanafunzi wa Chekechea kutumbukia Mtoni katika Jimbo la Hunan. Imeripotiwa na vyombo vya habari vya China.

SANCHEZ ATUA EMIRATES:- Mshambuliaji wa Kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez, amesaini Mkataba wa muda mrefu kuichezea Klabu ya Arsenal akitokea Klabu ya Barcelona.

PIGO KWA 'MZEE WA KUNG'ATA' SUAREZ:- Fifa yatupilia mbali rufaa ya FA ya Uruguay na mchezaji Luis Suarez ya kupinga kufungiwa mechi 9, baada ya nyota huyo kumng'ata beki wa Italia G. Chiellin.

KORTI KUHSMIS WODINI:- Utetezi wa Kesi ya EPA sasa kusikilizwa wodini Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa mtuhumiwa, Rajab Maranda, mnamo Agosti 11 kutokana na mtuhumiwa huyo kushindwa kuketi. Imeamuriwa na Mahakam ya Kisutu.

MAKOMBORA YARINDIMA GAZA:- Zaidi ya watu 80, wafa na 600 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yanayoendelea mjini Gaza, huku kundi la Hamas likizidi kuwarushia Waisraeli makombora.

MBIO ZA URAIS TANZANIA 2015:- Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema kuwa atagombea Urais katika uchaguzi wa 2015, iwapo wananchi watamtaka kufanya hivyo, kwani uwezo anao. Sumaye amesema hayo wakati akiwa katika ziara Jijini Mwanza.

WIZI WA MITIHANI:- Wilaya ya Handeni imewashusha vyeo Wakuu wa Sekondari za Kwaludege, Kwankonje kwa kusababisha jumla ya wanafunzi 138 wa kidato cha nne kufutiwa matokeo ya 2013.

MAUAJI MKOANI LINDI:- Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wanawake waliouawa Wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi, ni kutokana na 'ugomvi wa kimapenzi', na mpaka sasa jumla ya kesi 3 kati ya 7, zimetua Mahakamani, amesema RPC R. Mzinga. 

WAKATI HUO HUO, Mwili wa mwanamke mmoja uliookotwa Wilayani Nachingwea jana umetambuliwa kwa jina la Zuhura Mtenda (32) Aidha mwili huo pia umegundulika kuwa alibakwa na kisha kutobolewa macho na kuingizwa vijiti katika sehemu zake za siri na kutupwa kichakani, ambapo hadi sasa jumla ya wanawake 7 wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35, wameuawa kikatili wilayani humo.

 Jana Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wakazi wa Linsi walizingira Kituo cha Polisi wakipinga mauaji ya kinamama baada ya kuokotwa mwili wa Bi Zuhura jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.