Habari za Punde

*KOZI YA UKOCHA LESENI A SASA KUFANYIKA AGOSTI

Kocha ya ukocha wa mpira wa miguu ya leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyokuwa ianze kesho (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa itafanyika mwezi ujao.

Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na kuendesha kozi hiyo itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.


Tarehe rasmi ya kuanza kozi hiyo itatangazwa wiki ijayo. Mwezi uliopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya leseni B iliyoshirikisha makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.